IFANYE NGOZI YAKO NYORORO KWA KUTUMIA CHUMVI

Wapenzi wasomaji,
Leo tunakuletea namna ya kufanya scrub kwa kutumia chumvi na maji ya baridi na kuonekana wa kisasa zaidi.

Utumiaji huu ni wa salama zaidi na watumiaji wamethibitisha swala hilo kwa asilimia 100%.

Chumvi ni kiungo muhimu kwa kila mlo pia inaumuhimu mkubwa katika urembo. je una fahamu kwamba chumvi unaweza kuitumia kama scurb na kukuacha ukiwa na ngozi ya kuvutia na nyororo?

Matatizo ya chunusi , ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata ngozi iliyokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kuwafanya watumie vipodozi ambavyo si salama kwa ngozi zao.

Kwa kulitambua hilo wataalamu wa urembo wa asili wamegundua kuwa chumvi ni scrub yenye gharama nafuu ambayo kila mtu anaweza kutumia tofauti na urembo mwingine wa ngozi. Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi japo kuwa si wengi wanalolifahamu hili unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha chumvi haiingii machoni pindi unapotumia.

MAHITAJI

Chumvi ya unga kijiko kimoja cha chakula

Jinsi ya kufanya

Nawa uso wako kwa maji safi ya kawaida kisha chukua kitambaa laini na safi chovya kwenye chumvi kisha sugua kwenye uso taratibu pia unaweza kutumia hata mwilini.

Baada ya kujipaka katika uso weka pembeni kitambaa kisha anza kujisungua kwa kutumia viganja vya mikono yako fanya hivyo hadi utakapoona taka zinatoka kisha kaa kama dakika 2/5 ukisha maliza osha kwa maji ya baridi.

Ni muhimu kufanya zoezi hili kwa wiki mara mbili kwani linasaidia kuondoa mikunjo na husafisha ngozi kabisa

Comments

Post a Comment