Mwanaume na mwanamke ni muhimu kuwa watanashati kwani kujipiga sopusopu ni jambo la busara sana ili kukuweka katika hali ya
utanashati na mwenye kuvutia muda wote kwa kuondoa uchafu pamoja kuondoa mafuta ambayo yana kawaida ya kutanda katika sura ya
binadamu.
Wengi hupenda kuita kitendo hicho scrub, kitendo hichi husaidia kuondoa chunusi,vipele na makovu na pia inapunguza mafuta usoni.
Uso unapokuwa na mafuta sana na kuyaondoa kunasaidia kupunguza vitu vingi pamoja na vipele na hata mabaka yaliyosababishwa na
vipele au chunusi zinazo tokana na uwepo wa mafuta mengi katika ngozi.
Pia unaweza kutumia scrub kwa njia ya mikono kwa kila baada ya siku tatu, na scrub ya mashine baada ya mwezi mmoja, scrub ya mkono
ni nzuri na unashauriwa kutafuta aina ya scrub inayokufaa kulingana na ngozi yako.
Kabla ya kufanya scrabu unatakiwa kusafisha uso wako mpaka uhakikishe kuwa
umetakata kisha chukua scrub na kuanza kusugua usoni taratibu kwa muda wa
dakika tano kisha nawa uso na unaweza kupaka losheni au poda baada ya
kunawa.
Paka scrub usoni na pia shingoni kama utapenda ,sugua uso kwa kutoa
taka.chukua taulo, unashauriwa kutembelea saluni za kisasa kwa ajili ya
kuufanyia facial uso wako, unaweza kutafuta sabuni ya ukwaju na ukawa
unanawa uso asubuhi na jioni hii kuondoa upele, chunusi na mabaka usoni.
Comments
Post a Comment