WHO YATAJA SABABU KUU 8 ZINAZOFANYA WANAUME WENGI KUCHEPUKA

Image result for kwanini wanaume wanachepuka



Kama wewe ni mdada basi hii itakusaidia sana kulinda mahusiano yako na kama wewe ni mshkaji  unaechepuka basi utajua upo kwenye kundi gani. Hizi ni sababu 8 kwanini wanaume wengi huchepuka….
1. Vurugu na ugomvi katika mahusiano
Kugombana ni kitu cha kawaida katika mahusiano lakini inapokua ni mara kwa mara basi mwanaume huwa anakosa furaha na kuwa mwenye huzuni. Katika hali hii kuna machaguo mawili ambayo mwanaume anaweza kuyafanya ambayo ni kuendelea kugombana au kuchepuka kwenye utulivu.

2. Wanaume wanaochepuka wengi wanahusishwa na kuboreka
Wanaume wengi huhisi maisha ya mahusiano na mtu mmoja kama yanachosha na kukosa kitu kipya. Huu ndio mwanzo wa kuchepuka na kutafuta kitu kipya.

3. Wanaume  wengi wanaochepuka hupenda utundu kitandani
Yes, mapenzi ni sehemu kubwa ya mahusiano na itaendelea kua hivyo. Kuna wanaume wanaopenda kujaribisha mambo kibao kwenye mapenzi na kama wakiona hauwezi au hauna vigezo basi huchepuka kutafuta mtu anayeweza kumudu utundu wake.

4. Wanaume wanaochepuka hawajaridhika kihisia
Pale demu anapokua busy labda na kazi au na marafiki zake au na familia humuacha mwanaume katika hali mbaya kihisia kwani wanaume wengi wanapendwa kuonyeshwa upendo kila saa na kuonyeshwa kwamba wanajali juhudi zao za kuendeleza mahusiano. Mara nyingine mademu hujaribu sana kuonyesha upendo lakini pale inapokua mwanaume hana hisia basi ndio shida inapoanzia hapo.

5. Wanaume wengi wanaochepuka hutokana na historia yao
Kama jamaa alikua na mademu kama 6 kwa kipindi cha miaka 3 aliyokua chuo  basi ni rahisi kuwarudia pale anapopata hiyo nafasi. Au unakuta maranyingine mwanaume amekulia kwenye mazingira ambayo amemuona mzee akichepuka mara kibao basi nayeye anajifunza na kutoona kama ni kosa kuchepuka.

6. Wanaume wengi wanaochepuka wanamademu wachepukaji !
Wanaume wengi pia huchepuka kama njia ya kulipika kisasi sababu mademu wao nao wanachepuka. Hata kama wmademu zao wakitubu kwamba walikua wanachepuka lakini bado wanaume wengi huendeleza haka kamchezo.

7. Wanaume huchepuka ili kumtosa mwanamke
Ushawahi kukaa na demu ambae unatamani umwambie kwamba wewe na yeye basi lakini unashindwa kumwambia kwa maneno basi mwisho wa siku unaamua kutumia vitendo na pale anapogundua kwamba unachepuka basi huo ndio unakua mwisho wenu.

8. Wanaume wanaochepuka hukosa hali ya kupendwa
Wanaume wengi hupenda kuhisi hali ya kuhitajika kutoka kwa wanawake, pale unapohisi kwamba sio mwanamke yoyote tu bali demu wake akuhitaji basi inakua ni shiiida.

Basi ushauri wa mwisho ni kwa wanawake kuyazingatia haya na kwa wanaume kuacha michepuko  , ni bora kumwambia mtu ukweli.

Comments