Nywele zimekuwa kivutio kikubwa hasa kwa mwanamke kwani kiasi fulani huchangia kumfanya muhusika aonekane mrembo na wa kuvutia zaidi.
Kutokana na matumizi ya dawa zenye kemikali, wanawake wengi wamejikuta wakiwa na tatizo la nywele zao kukatika na kupoteza mvuto wake wa asili.
Hilo huchangia kuzifanya nywele zikose afya na uhalisia wake, hali inayowakosesha raha wanawake wengi, hasa wanaozingatia masuala ya urembo. Leo tutaangalia namna ya kuboresha mwonekano wa nywele kwa kutumia njia rahisi, nafuu ambayo yoyte anaweza kuimudu.
Wengi wanaweza kushangaa, lakini tui la nazi ni njia bora ya kuimrisha afya ya nywele na kuzifanya zijae vizuri kichwani na kuvutia .
Namna ya kufanya
Tafuta nazi yako iliyokomaa vizuri, kisha ikune kwa utaratibu ili utoe vipande vidogodogo na kuifanya iwe laini.
Baada ya hapo, weka maji kidogo na uchuje tui katika chombo kisafi, hakikisha unapata tui la kwanza likiwa zito kabla halijakatika.
Osha nywele zako kwa maji safi yenye uvuguvugu mpaka uhakikishe hakuna mafuta wala uchafu ulioganda kwenye ngozi ya kichwa.
Baada ya kufuta maji yote kichwani, chukua tui lako la nazi, anza kupaka kwa kuchambua nywele kidogo kidogo hadi uhakikishe zote zimekolea vizuri.
Vaa kofia ya plastiki au mfuko kwa muda wa saa moja kuliacha tui la nazi lifanye kazi vizuri kichwani. Baada ya hapo, osha nywele zako, kausha na upake mafuta ambayo hayatakuwa na kemikali.
Ukifanya hivi kila wiki kwa hakika nywelezako zitaimarika na kuwa na afya kwa haraka zaidi. Njia hii inaweza kuwa rahisi kuliko zote kutokana na unafuu wake na upatikanaji wa nazi kwa kuwa kila mmoja anaweza kupata.
Comments
Post a Comment