Urembo unajumuisha mambo mengi kwa mwanamke tofauti na dhana za
watu wengi wanaofikiri kwamba urembo ni kuvaa vizuri, kuonekana vizuri na hata
manukato mazuri, kuwa na umbo zuri, na jinsi unavyoonekana kutokana na umbo
lako. La hasha hivi ni vidokezo vya urembo kwa mwanamke.
Urembo halisi ni amani na utulivu uliopo ndani yako, hali hii ina faida katika moyo wako na mwili wako pia. Jambo la msingi hapa ni kuwa na amani kwa kuepukana na msongo wa mawazo na kuwa mwenye furaha muda wote. Hali ya msongo wa mawazo (stress) huleta maradhi mbalimbali kama vidonda vya tumbo(gastriculcers),shinikizo la damu(blood pressure) namengi.
Katika maisha ya mwanamke yeyote mwenye kupenda urembo na muonekano mzuri ni pamoja na kuepukana na magonjwa yanayoepukika kwa njia ya kua na amani na furaha muda wote kwa kujenga sura nzuri, umbo zuri lenye kupendeza pale unapovaa nguo ya aina yoyote au kupaka vipodozi vya aina yoyote ile.
Je ni kiasi gani cha fedha tunatumia kila mwaka kununua nguo mpya, viatu vya gharama, vipodozi na mikoba? Bila shaka ni gharama kubwa lakini je, kuna gharama gani tunatumia kujenga furaha na amani ndani yetu? Jibu ni rahisi tu furaha na amani ni wewe mwenyewe pasipo gharama yoyote ile. Maswali haya yatakufanya wewe kama mwanamke mpenda urembo kupata njia thabiti za kuongeza urembo.

ITAENDELEA
Comments
Post a Comment